JE NIFANYE NINI KAMA MAZIWA HAYATOKI

 KUTOTOKA KWA MAZIWA YA KUTOSHA KUNATOKANA NA FACTOR KUBWA ZIFUATAZO:


1. CHAKULA: Aina ya chakula unashauliwa mama anayenyonyesha kula vyakula anavovipenda wakati huohuo vyeny wingi wa protein. Zaidi sana unachojisikia kula we kula tu


2. STRESS: hii ni kikwazo kikubwa sana kwa mama anayenyonyesha stress hupunguza uzalishaji wa homoni ya prolactin ambayo husababisha kuzalisha maziwa kwa wingi na homoni ya Oxitocin hufanya kazi ya kuyaachia kutoka homoni hizi mbili hufanya maziwa kutoka kwa wingi.

Unachotakiwa kufanya ni wakati wa kunyonyesha kama mume wako yuko karibu jaribu kumwambia akusugue mabegani taratibu hii itakusaidia kurilax

Lakini kama hauna mume au hayupo wewe wakati wa kunyonyesha sikiliza mziki mzuri uupendao na uwe unakunywa kinywaji chochote ukipendacho (Ila isiwe bia au kilevi chochote hapana)


3. GENETIC: Hii ni kwa wachache sana endapo umetumia njia zote na hakuna mabadiliko basi ujue Ni genetic yaa Yaani kurithi muulize mama yako au mama mdogo au bibi je kuna yeyote mwenye tatizo hili??


4. KUKWAMA KWA MAZIWA: hii hutokea kwenye mirija inayotoa maziwa endapo imezima yaani kwenye matiti na hutokea endapo labda mama hanyonyeshi mara kwa mara matiti yamejaa ila hayatoi maziwa mama anashauliwa kumnyonyesha mtoto muda wowote mtoto akipenda lakini kuna watoto wengine wanapenda sana kulala hasa kipindi cha joto basi umuamshe walau kila baada ya masaa mawili 

Hii endapo kuna shida ya matiti lakini kama hakuna shida basi mnyonyeshe anapohitaji mda wowote

Comments

Popular posts from this blog

DALILI ZA UCHUNGU

HATUA ZA KINGA KWA MAMA MJAMZITO